June 20, 2016

Yanga yaanza vibaya CAF jana baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mo bejaia


Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Yanga wa Kundi A lenye timu za TP Mazembe ya Kongo, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, katika mchezo huo Yanga wamekubali kufungwa jumla ya goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Yacine Sahli dakika ya 20 ya mchezo ila Yanga walipata pigo baada ya Mwinyi Haji kuoneshwa kadi nyekundu kwa kucheza faulo.