June 20, 2016

Watu sita wa familia moja wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada kuugua ugonjwa usiojulikana.

Dodoma. Watu sita wa familia moja wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada kuugua ugonjwa usiojulikana.

Akizungumza katika wodi hiyo, baba wa familia hiyo, mkazi wa Mwaikisabe, Salim Rashid amesema: "Tulikula nyama tuliyopewa na jirani yetu na jioni tukala ugali na maziwa. Tulianza kuugua na baada ya siku tatu kutapika na kuharisha."

Nje ya wodi walimolazwa wagonjwa hao, kumefungwa utepe unaoonyesha mwisho wa watu kukanyaga.

Wanaoruhusiwa kuingia ndani ya wodi hiyo wanakanyaga maji yaliyowekwa dawa na hawaruhusiwi kushika chochote kile kilichomo wala kumgusa mgonjwa.

Muuguzi katika wodi hiyo, Stella Joseph amemweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu kuwa wamepowapokea wagonjwa hao wakiwa wanaharisha na kutapika, lakini kwa sasa wamefunga.