June 20, 2016

Uzalendo wa dhati umeonekana rwanda jana, watoto wa raisi kagame waingia dimbani siku ya kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari.

Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 katika mechi ya kuadhimisha miaka 22 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Mchuano huo wa kumbukumbu, kati ya Rwanda na Morocco ulioandaliwa katika uwanja wa Amahoro, mjini Kigali ulikamilika kwa sare ya goli moja.

Ingawa wote wawili hawakukamilisha mechi hiyo. Kocha wa Rwanda Kayiranga Jean Baptista aliwapa nafasi ikiwa ni mechi yao ya kwanza kuvaa sare ya timu ya taifa ya soka.

Ian Kigenza Kagame alijumuishwa katika kikosi kilichoanza kabla ya kumpisha Park Udahemuka kunako dakika ya 27.