June 20, 2016

Ukubwa wa heshima ya mitiani Algeria imepelekea kufungwa kwa muda mitandao ya jamii.

Algeria imefunga kwa muda mitandao ya kijamii kote nchini katika jitihada za kuzuia wizi wa mitihani ya shule za upili.

Karibu nusu ya wanafunzi walilazimishwa kurudia mtihani huo kuanzia jana Jumapili, baada ya mtihani wa kwanza kukumbwa na udanganyifu kwa njia ya mitandao.

Wanafunzi wengi walifanikiwa kupata maswali kwa njia ya mtandao wa Facebook na mitandao mingine kabla ya kufanyika kwa mtihani huo.

Hatua ya kufunga mitandao ya kijamii ililenga kuwalinda wanafunzi kutokana na kuchapisha maswali yasiyo sahihi kupitia kwa mitandao hiyo.