June 20, 2016

KWA WALIO NA WATARAJIAO KUWA WATUMISHI WA UMMA:

Serikali imetoa waraka tarehe 13/6/2016, unaoonyesha yafuatayo;

1. Kusitisha ajira zote mpya.

2. Kusitisha nyongeza zote za mishahara.

3. Kusitisha utoaji vibali kwa watumishi waliokuwa likizo bila malipo kurudi kazini.

4. Kusitisha vibali kwa watumishi wanaoacha kazi serikalini na kisha kurudi tena serikalini kwa cheki namba za awali.

5. Kusitisha utoaji vibali vya kurudi kazini kwa watumishi wanaochukua likizo bila malipo.

6. Kusitisha utaratibu wa watumishi kuhama ofisi moja kwenda nyingine kuliko na mshahara mkubwa zaidi ya ule wa ofisi ya awali.

7. Kusitisha pia miundo yote mipya ya utumishi.

Mpaka hapo itakapojulishwa zaidi.