June 20, 2016

Je! Ulimmiss Askofu ngwajima kwenye headlines? Leo ana hii na siasa baada ya kutafutwa na polisi akabizi kanisa.

Kanisa la Ufufuo na Uzima, jana limeongozwa na mchungaji Edward Adriano badala ya Askofu Josephat Gwajima ambaye anatafutwa na polisi.

Hata hivyo, mchungaji Adriano amesema jana kuwa Askofu Gwajima amesafiri, bado hajarudi.

Msako huo wa Askofu Gwajima umekuja baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake akitaka Rais mstaafu, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake.

Jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema suala la Askofu Gwajima atalizungumza leo.

Alhamisi iliyopita polisi walizingira nyumbani kwa askogu huyo kwa saa saba, wakitaka kumkamata bila mafanikio.